Kocha wa Arsenal ya Uingereza Arsene Wenger, amesema kuwa mshambulizi Mesut Ozil angali anajutia kukosa kufunga penalti dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi kuu barani ulaya Bayern Munich jumanne iiyopita.
Ozil, mwenye umri wa miaka 25,alilazimika kuwaomba radhi mashabiki wa Arsenal kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.
Ozil,alisajiliwa mapema msimu huu kwa kitita kikubwa zaidi na kocha Wenger.
Arsenal, inashikilia nafasi ya pili katika ligi kuu ya premia ya Uingereza ikiwa na jumla ya alama 56 moja nyuma ya vinara Chelsea .
Arsenal inaikaribisha Sunderland jumamosi katika uwanja wa Emirati .
No comments:
Post a Comment