Sunday, March 9, 2014

Wenger kucheza mchezo wake wa 1000 na Jose Mourinho English Premium League

Wenger v Mourinho

Kati ya michezo ya ligi kuu ya Uingereza isiyopendwa na kocha Arsene Wenger ni dhidi ya Chelsea ya Mourinho. Wakiwa mahasimu wakubwa, Bosi Arsene Wenger anahofu huenda Morinho akaifanya siku yake ikajawa na majonzi. Siku za hivi karibuni Morinho amaemwelezea Wenger kama kocha mwenye mafanikio ya kufeli zaidi katika ligi kuu ya England. Morinho amesema kwamba Wenger anapoteza muda kwa kuiga mchezo wa Barcelona usiowezekana katika mazingira ya Uingereza. Wenger atafikisha mchezo wa 1000 akiwa na Arsenal katika mchezo dhidi ya Chelsea. Kwa sasa Arsenal iko nafasi ya tatu nyuma ya Chesea na Liverpool. Jana jumamosi ilifanikiwa kuelekea nusu fainali ya kombe la FA baada ya kuibwaga Everton mabao 4 - 1.

No comments:

Post a Comment