Kati ya michezo ya ligi kuu ya Uingereza isiyopendwa na kocha Arsene Wenger ni dhidi ya Chelsea ya Mourinho. Wakiwa mahasimu wakubwa, Bosi Arsene Wenger anahofu huenda Morinho akaifanya siku yake ikajawa na majonzi. Siku za hivi karibuni Morinho amaemwelezea Wenger kama kocha mwenye mafanikio ya kufeli zaidi katika ligi kuu ya England. Morinho amesema kwamba Wenger anapoteza muda kwa kuiga mchezo wa Barcelona usiowezekana katika mazingira ya Uingereza. Wenger atafikisha mchezo wa 1000 akiwa na Arsenal katika mchezo dhidi ya Chelsea. Kwa sasa Arsenal iko nafasi ya tatu nyuma ya Chesea na Liverpool. Jana jumamosi ilifanikiwa kuelekea nusu fainali ya kombe la FA baada ya kuibwaga Everton mabao 4 - 1.
Sunday, March 9, 2014
Saturday, March 8, 2014
Arsenal yaelekea Wembley
Magoli manne yametosha kuipeleka Arsenal nusu fainali ya FA itakayochezewa katika uwanja wa Wembley. Ikiwa inacheza na Everton mchezo ulionekana kuwa mgumu kwa Arsenal katika kipindi cha kwanza, japo mambo yalibadilika kipindi cha pili baada ya Rosicky na Giroud kuchukua nafasi za Chamberlain na Sanogo. Arsenal ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Ozil kabla ya Lukaku kusawazisha katika kipindi cha kwanza. Dakika ya 70 Arsenal ilipata bao la pili kupitia kwa Arteta kwa mkwaju wa Penalt.
Dakika 10 za mwisho Giroud alipachika wavuni magoli 2 na mechi ikaisha ubao ukisomeka 4 - 1.
Kwa habari zaidi tembelea:-
Thursday, March 6, 2014
Jack Wilshere nje wiki sita
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal Jack Wilshere atakosa kucheza wiki sita baada ya kupata jeraha la mguu katika mechi aliyochezea England hapo juzi iliposhinda Denmark bao moja kwa bila. Kwa sababu hiyo atakosa mchuano wa FA wa robo fainali hapo kesho dhidi ya Everton na Jumanne ijayo atatazama tu timu yake ikicheza na Bayern Munich katika kombe la kilabu bingwa barani ulaya.
Si hayo tu atakosa mechi nne muhimu za ligii ya England kati ya Chelsea, Manchester City, Swansea na Tottenham ambazo zinacheza mwezi huu.
Wednesday, March 5, 2014
Carles Puyol Kutimka Barcelona
Nahodha wa klabu ya Barcelona Carles Puyol ametangaza atawahama mabingwa hao wa Hispania mwishoni mwa msimu huu.
Puyol mwenye umri wa miaka 35 aliibukia kutoka vikosi vya vijana wa Barcelona na kujiunga na kikosi kikuu mwaka 1999.
Monday, March 3, 2014
Mkenya Lupita Nyong'o anyakua tuzo ya Oscar
Kama ilivyokuwa imetarajiwa na wengi mwigizaji mashuhuri kutoka Kenya Lupita Nyong'o amenyakuwa tuzo la Oscar la mwigizaji msaidizi wa kike kwa jukumu lake la kuelezea masaibu ya Patseh katika filamu ya utumwa ya ''12 Years A Slave.''
Baada ya kupokea tuzo hilo Lupita amesema " Haikwepi mawazo yangu kwamba hata dakika moja ya furaha katika maisha yangu ni shukran na maumivu makubwa kwa mtu mwingine.''
Kisha Lupita akaongeza kusema, " Na iwe ukumbusho kwangu na kila mtoto kwamba kokote unakotoka, ndoto zako ni halisi.''
Mwigizaji Jared Leto alinyakuwa tuzo la mwigizaji bora msaidizi wa kiume kwa jukumu lake la kuelezea maisha ya mwanamke aliye na jinsia mbili aliyekuwa na akiishi na virusi vya HIV katika filamu Dallas Buyers Club.
Alilazimika kupunguza uzani kwa kipindi kifupi ili kuigiza.
Sherehe ya kutolewa kwa tuzo hizo zimefanyika mjini Los Angeles nchini Marekani.
Subscribe to:
Posts (Atom)